Watu waaminifu wa Iran ya Kiislamu leo hii wameonyesha kwamba damu ya Mashujaa – Kuanzia Makamanda jasiri na Wanasayansi wa Nyuklia hadi Watoto na raia wasio na hatia – ni mbegu iliyopandwa katika ardhi ya Taifa hili, ambayo itazaa mti mkubwa wa heshima na ushindi.
Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA-; Leo tarehe, 7 Tir, 1404 (Shamsi) sawa na tarehe (28 Juni, 2025), mitaa ya Tehran – moyo wa Mapinduzi ya Kiislamu – imeshuhudia moja ya maonyesho makubwa kabisa ya umoja na mapambano. Hafla ya mazishi na maziko ya miili mitukufu ya mashujaa waliouawa katika mashambulizi ya kikatili ya utawala haram wa Kizayuni dhidi ya ardhi ya Iran, imefanyika kuanzia Uwanja wa Mapinduzi ya Kiislamu hadi Uwanja wa Uhuru, kwa ushiriki wa mamilioni ya watu waliokuwa katika hali ya huzuni na hasira.
Katika siku hii ya kihistoria, watu wa Tehran kutoka kila tabaka na kila rika, wakiwa na macho yenye machozi na mioyo iliyojaa hasira na azimio, walijitokeza kuaga mashahidi wao – kuanzia makamanda jasiri na wanasayansi wa nyuklia hadi raia wasio na hatia, wakiwemo watoto na wanawake wasiokuwa na hatia – na kuwapelekea adui wa Taifa hili (meseji) ujumbe thabiti.
Hasira na Huzuni ya Taifa Katika Maombolezo ya Mashahidi
Kuanzia alfajiri ya leo, mitaa inayoelekea Uwanja wa Mapinduzi ya Kiislamu ilikuwa imejaa umati mkubwa wa watu waliokuwa wamebeba bendera nyekundu za Imam Hussein (as), picha za Mashahidi, na Mabango yenye kauli mbiu kama "Kifo kwa Israel" na "Kifo kwa Marekani."
Kati ya wingi huo mkubwa wa watu, picha za watoto wadogo waliouawa katika mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni dhidi ya makazi ya raia na miundombinu ya kiraia ya Tehran, ziligusa mioyo ya watu zaidi ya yote. Majina na picha za Rayan wa miezi miwili, Fatimah Sadati mwenye umri wa miaka 8, Reyhaneh Sadati wa miaka 15, Baran Eshraghi, Parnia Abbasi, na watoto wengine Mashahidi – zilibeba kumbukumbu ya milele pamoja na makamanda waliouawa kishahidi.
Hiki ni kilio cha mama mmoja aliyekuwa katika huzuni kuu, ambapo alisikika akisema:
"Binti yangu alikuwa na miaka mitano tu. Alikuwa amelala nyumbani kwake wakati kombora la Kizayuni lilipobomoa nyumba yetu. Huu ni uadui wa aina gani unaowalenga watoto?".
Miili midogo ya watoto waliowekwa kwenye majeneza ilisababisha machozi kumwagika usoni mwa watu, na kauli mbiu zilisikika kwa sauti ya majonzi zikisema:
"Israel imeangamia" na "Mzayuni muuaji wa watoto, jibu lako ni damu."
Ushiriki Mkubwa wa Wananchi; Ushujaa na Hamasa ya Umoja wa A'shura
Ushiriki huu wa kihistoria ulikuwa taswira ya kipekee ya umoja wa A'shura. Uwanja wa Mapinduzi ya Kiislamu, uliopambwa kwa michoro ya mashujaa na ujumbe wa mapambano, ulibadilika na kuwa jukwaa la heshima na nguvu. Wananchi kutoka tabaka mbalimbali – kuanzia wafanyakazi na wanafunzi hadi Maulamaa na familia za Mashahidi – walifika wakiwa na bendera za Iran na picha za mashujaa waliouawa Shahidi kama vile Jenerali Mohammad Baqeri, Jenerali Hossein Salami, Jenerali Gholam-Ali Rashid, Jenerali Amir-Ali Hajizadeh, pamoja na wanasayansi wa nyuklia kama Fereydoon Abbasi na Mohammad-Mehdi Tehranchi.
Viongozi wakuu wa Serikali pia walihudhuria, akiwemo Rais wa Jamhuri, Dkt. Pezeshkian, Jenerali Esmail Qaani, Mohammad-Baqer Qalibaf, Gholamhossein Mohseni Ejei, na Abbas Araghchi – wakisimama bega kwa bega na wananchi – wakionyesha mshikamano wa kina kati ya Taifa na uongozi wa Kiislamu.
Wananchi waliokuwa katika maombolezo walituma ujumbe wao kwa viongozi uliosema:
"Si suluhu, si kujisalimisha – ni vita na Marekani" – kauli mbiu iliyotoka ndani kabisa ya nafsi za watu dhidi ya jinai na hila za Marekani.
Mwandishi wa Habari wa Shirika la Habari la CNN akichukua picha selfie katika mkusanyiko mkubwa na wananchi wa Iran waliojitokeza kwa wingi kushiriki katika mazishi na maziko ya makanda wao wa kijeshi, wanasayansi wa nyuklia, na watoto na wanawake waliouawa kishahidi katika shambulizi la kigaidi la Israel.
Shambulizi hilo la kigaidi la Israel ndilo lililoibua vita vya siku kumi na mbili baina ya Iran na Israel, ambapo Iran ilichukua hatua kali mno ya kuishambulia kwa makombora hatari yenye teknolojia ya hali ya juu, ambalo israel haikulitarajia na badala yake ili kujiokoa na mashambulizi ya Iran ikaomba Marekani iisaidie kuomba suluhu baina yake na Iran ya kusitisha mashambulizi ya Iran dhidi ya utawala huo. Marekani iliiomba Qatar iingilie kati kwa kuwasiliana na Iran na kuiomba Iran isitishe mashambulizi yake dhidi ya Israel, na kwa sababu uislamu unasema adui akiomba suluhu mkubalie, ndipo Iran ilipositisha operesheni yake ya Ahadi ya Kweli 3, iliyodumu kwa muda wa siku 12 ambazo zilitosha kabisa kuichakaza Israel kila kona kwa kuitwanga katika maeneo nyeti mbalimbali ya kijeshi na kiistratejia, jambo lililoifanya Israel kuchanganyikiwa na walowezi wa kizayuni zaidi ya milioni mbili kukimbilia katika kisiwa cha Cyprus na wengi kukimbilia ulaya walikotokea.
Your Comment